Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:51

Blinken atangaza mpango wa Biden kukutana na viongozi wa Afrika


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto, akikaribishwa na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, kulia, kabla ya mkutano wao katika ikulu ya Rais Abuja, Nigeria, Nov. 18, 2021.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto, akikaribishwa na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, kulia, kabla ya mkutano wao katika ikulu ya Rais Abuja, Nigeria, Nov. 18, 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitangaza leo Ijumaa kuwa Rais wa Marekani Joe Biden anapanga kuanda mkutano na viongozi wa Afrika ili kuonyesha dhamira ya Marekani kwa bara hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitangaza Ijumaa kuwa Rais wa Marekani Joe Biden anapanga kuandaa mkutano na viongozi wa Afrika ili kuonyesha dhamira ya Marekani kwa bara hilo.

Blinken alisema katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kwamba Rais Biden anakusudia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika ili kuendesha aina ya diplomasia na ushirikiano wa hali ya juu ambao unaweza kubadilisha uhusiano na kufanya ushirikiano wenye ufanisi iwezekanavyo .

Blinken, ambaye yuko katika ziara yake ya kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kama waziri wa mambo ya nje, hakutoa tarehe ya mkutano huo.

Hatua hiyo iinatokea wakati China ikiongeza ushirikiano na Afrika ikiwa ni pamoja na kupitia mkutano mkuu mwezi huu nchini Senegal, ambapo Blinken anaongoza baadaye Ijumaa.

Washirika wa Marekani Ufaransa, Uingereza na Japan pia wamekuwa wakifanya mikutano ya mara kwa mara na viongozi wa Afrika.

Blinken alikutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari siku ya Alhamisi na kujadili usalama wa ndani na kikanda, na kurudi nyuma kidemokrasia Afrika Magharibi, ikiwa ni pamoja na jinsi Abuja ilivyoshughulikia maandamano ya kupinga ukatili wa polisi mwaka jana

XS
SM
MD
LG