Iran imekuwa ikikwamisha makubaliano ambayo yatairuhusu IAEA kuchunguza vinu vyake ambako chembechembe za uranium ziligunduliwa. Iran pia imekubali kurejesha kamera na vifaa vingine vya ufuatiliaji ambavyo viliondolewa kutoka katika maeneno hayo.
IAEA na Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran zimetoa taarifa ya pamoja Jumamosi zikisema “mikutano ya ngazi ya juu” wakati wa ziara ya siku mbili ya Grossi “ilishughulikia umuhimu wa kuchukua hatua ili kuwezesha kuimarisha ushirikiano, kuharakisha inavyopaswa azimio la masuala ya udhibiti yaliyokuwa hayajakamilika.”
Taarifa hiyo ilisema mazungumzo kati ya IAEA na Iran “yatafanyika kwa moyo wa ushirikiano, na kwa kufuata kikamilifu muongozo wa IAEA na haki na majukumu ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran, ikizingatia makubaliano kamili ya udhibiti huo.
Grossi alizungumza na waandishi Jumamosi huko Vienna. Akijibu swali la mwandishi wa VOA, Grossi alisema kuwa IAEA na shirika la Iran “wamekubaliana juu ya mambo mahsusi kadhaa” na kuwa IAEA itapewa “baadhi ya ruhusa” lakini haikuziorodhesha.
Alisema shirika lake “siku zote litakuwa wazi katika misingi ya mafanikio yake ambayo ana matumaini nayo.”
“Tunachukua hatua zenye mwelekeo sahihi,” Grossi alisema, “lakini sitaki kusikika kuwa na matumaini sana au kukata tamaa.”
“Nafikiri tuna kazi ngumu mbele yetu,” Grossi alisema, “kuna kazi nyingi mbele yetu kwa Iran na sisi wenyewe.