Iran ilikanusha ripoti Jumatatu kwamba inasindika madini ya Uranium hadi kufikia kiwango cha utengenezaji silaha. Hadi sasa hatujafanya jaribio lolote la kurutubisha zaidi ya asilimia 60. Uwepo wa chembe-chembe juu ya asilimia 60 ya usindikajii haimaanishi urutubishaji zaidi ya asilimia 60 msemaji wa shirika la nishati la Atomik la Iran, Behrouz kamalvandi alisema Jumatatu kulingana na shirika rasmi la habari la IRNA.
Ripoti ya Bloomberg News ya Jumapili ilisema wakaguzi kutoka shirika la kimataifa la atomic waligundua Uranium iliyorutubishwa hadi asilimia 84. Uranium lazima irutubishwe hadi karibu asilimia 90 kwa bomu la nyuklia. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu wakati wa ziara yake nchini Uturuki kwamba Marekani ilikuwa na mawasiliano ya karibu na IAEA na inafanya kazi kupata taarifa zaidi kuhusu hali hiyo.
Hili litakuwa jambo makini sana, alisema Blinken. IAEA ilisema kwenye Tweet hapo Jumapili kwamba ilifahamu ripoti kuhusiana na viwango vya urutubishaji wa uranium nchini Iran.
Facebook Forum