Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:04

Jeshi la Uingereza lakamata silaha kwenye Ghuba ya Oman


Jeshi la wanamaji la Uingereza, Alhamisi limesema vikosi vyake vilikamata makombora ya kushambulia vifaru ya Iran na vifaa vya makombora ya mbali kutoka kwenye boti ndogo katika Ghuba ya Oman.

Uingereza haikutaja mahali ambapo silaha hizo ziikuwa zinapelekwa, lakini jeshi la Marekani, ambalo lilisema lilitoa msaada wa kijasusi, na uchunguzi kwa operesheni hiyo, lilisema utekaji nyara huo ulifanyika katika njia ambayo kihistoria ilitumika kusafirisha silaha kinyume cha sheria kwenda Yemen.

Ni moja ya msururu wa shehena zilizonaswa na vikosi vya magharibi vinavyosema Iran imewapa silaha waasi wa kihouthi nchini Yemen, madai ambayo Iran inakanusha.

XS
SM
MD
LG