Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:08

Iran imewaamuru wanadiplomasia wawili wa Ujerumani kuondoka nchini humo


Nasser Kanani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran
Nasser Kanani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran

Hatua ya Ujerumani kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Iran ilikuja kufuatia kupinga hatua ya Iran kumpatia hukumu ya kifo raia wa Ujerumani Jamshid Sharmahd

Iran leo Jumatano iliwaamuru wanadiplomasia wawili wa Ujerumani kuondoka nchini humo ikiwa ni majibu kwa hatua kama hiyo iliyofanywa na ujerumani wiki iliyopita.

Hatua ya Ujerumani kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Iran ilikuja kufuatia kupinga hatua ya Iran kumpatia hukumu ya kifo raia wa Ujerumani Jamshid Sharmahd. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Nasser Kanani alisema Jumatano kwamba Ujerumani inaingilia masuala ya ndani na ya kimahakama ya Iran.

Iran ilimshutumu Sharmahd kwa kuongoza tawi lenye silaha la kundi linalounga mkono utawala wa kifalme, ambalo familia yake ilikanusha. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alisema baada ya hukumu hiyo wiki iliyopita kwamba Sharmahd alikamatwa katika mazingira ya kutatanisha na kwamba "hajawahi hata kuwa na mfanano wa kesi ya haki".

XS
SM
MD
LG