Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:17
VOA Direct Packages

Uingereza yasema huenda Russia imepungukiwa na silaha za anga kutoka Iran


Silaha iliyorushwa angani na Russia kwenye picha ya maktaba
Silaha iliyorushwa angani na Russia kwenye picha ya maktaba

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema Jumamosi kupitia taarifa ya kipelelezi kwamba  huenda Russia imepungukiwa na  silaha za mashambulizi ya anga aina ya OWA UAV zisizokuwa na rubani kutoka Iran.

Ripoti hiyo imeongeza kusema kwamba silaha hizo hazijatumika tangu Februari 15 wakati takriban 24 zikikiwa zimetunguliwa kati ya Januari na mapema mwezi huu.

Wizara hiyo imeongeza kusema kwamba huenda Russia ikaagiza silaha ziadi za aina hiyo licha ya rekodi yake mbaya ya kushindwa kupiga maeneo waliyoyalenga.

Ijumaa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine, Ikulu ya Marekani ilitangaza msaada wa kijeshi wa dola bilioni mbili kutoka Pentagon, kwa jeshi la Ukraine, ili kujilinda kutokana na vikosi vya Russia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakati wa maadhimisho hayo alisema kwamba vifo vingi vya watu wa Ukraine vilivyosababishwa na Russia visiachwe bila ya wahusika kuwajibishwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken pia amerejea kusisitia nia ya dhati ya Marekani kuisaidia Ukraine katika miundombimu.

XS
SM
MD
LG