Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 21:44

Hisia ya kufunguliwa mashtaka Trump yaonyesha kuwepo mgawanyiko wa kisiasa Marekani


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Hisia ya kufunguliwa mashtaka Donald Trump, akiwa ni rais wa kwanza wa  zamani wa Marekani, ilikuwa imetabiriwa katika bunge lenye mgawanyiko wa siasa za  Marekani.

Warepublikan wenzake walimshambulia mwendesha mashtaka kwa kile walichodai ni kitendo kilichoelemea upande mmoja, wakati Wademokrat wakishikilia kuwa hakuna mtu yeyote ambaye ataruhusiwa awe juu ya sheria.

Hata Warepublikan wanaowania uteuzi wa kugombea urais katika uchaguzi wa 2024 dhidi ya Trump walimtetea baada ya jopo la mahakama huko New York kumfungulia mashtaka Trump yanayohusiana na malipo ya dola 130,000 kumnyamazisha mcheza filamu za ngono ambaye alidai alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Trump muongo moja uliopita. Trump ameendelea kukanusha madai hayo ya mcheza filamu za ngono, Stormy Daniels.

Gavana wa Florida Ron DeSantis, ambaye hajatangaza azma yake ya kuwania urais 2024 lakini kitaifa kura za maoni zinaonyesha yuko nyuma ya Trump katika uteuzi, katika ujumbe wake wa Twitter alimtuhumu mwendesha mashtaka wa New York Alvin Bragg, mdemocrat, kwa kutumia mfumo wa sheria “ kutekeleza ajenda ya kisiasa” ambapo alisema “ inapindua utawala wa sheria kichwa chini.”

Ron DeSantis
Ron DeSantis

DeSantis alisema hatoshirikiana na maafisa wa New York kumpeleka Trump kutoka Florida ili akafunguliwe mashtaka, licha ya kuwa pengine halitokuwa tatizo katika tukio lolote. Wakili wa Trump amesema kuwa rais wa zamani atasafiri kwa ndege kwenda New York kujisalimisha.

Nikki Haley, balozi wa zamani wa Trump katika Umoja wa Mataifa ambaye ametangaza azma ya kugombea urais mwaka 2024, alisema kuhusu kufunguliwa mashtaka Trump, “Hili ni kuhusu ulipizaji kisasi kuliko kutafuta haki.”

Nikki Haley
Nikki Haley

Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa utawala wa Trump na mgombea mwingine mtarajiwa wa urais, alimshutumu mwendesha mashtaka kwa “kutumia hujuma ya kisiasa.”

Mike Pompeo
Mike Pompeo

Seneta Mrepublikan wa South Carolina Tim Scott, ambaye ni mgombea mtarajiwa mwingine, alisema katika taarifa yake, “Huyu muendesha mshtaka wa New York anayeunga mkono uhalifu ameshindwa kupitisha sheria kwa wahalifu, lakini anatumia sheria kama silaha dhidi ya maadui wa kisiasa. Huu ni uzembe, na hili halitakiwi kufanyika katika nchi bora kabisa duniani.”

Tim Scott
Tim Scott

Mahasimu Wademokratik dhidi ya Trump walichukua mtizamo mwingine, wakisema mtu yeyote hatakiwi kuwa na uwezo wa kukwepa kushtakiwa kama amefanya makosa lakini afikishwe mahakamani siku moja kujibu mashtaka hayo.

Nancy Pelosi, spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, aliandika kwenye Twitter, “Jopo la Mahakama limefanyia kazi ukweli uliopo na sheria iliyopo. Hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria, na kila mtu ana haki ya kuthibitisha mahakamani hana makosa.”

Nancy Pelosi
Nancy Pelosi

“Ni matumaini yangu, Rais wa zamani huyo kwa usalama ataheshimu mfumo huo, unaompa haki hiyo,” aliongeza.

Chuck Schumer
Chuck Schumer

Kiongozi Mdemokrat wa waliowengi katika Baraza la Seneti, Chuck Schumer, alisema katika taarifa yake: “Bwana Trump yuko chini ya sheria kama ilivyo Mmarekani yeyote. Ataweza kufikia mfumo wa sheria na jopo la mahakama, na siyo siasa, kufahamu hatma yake kulingana na ukweli na sheria. Hakutakiwi kuwa na ushawishi wa nje wa kisiasa, vitisho, au uingiliaji kati wa kesi. Nina wahimiza wote wakosoaji wa Bw Trump na wanaomuunga mkono kuachia mchakato kwa mujibu wa sheria kuchukua mkondo wake kwa amani.”

Trang Le wa Orlando, kulia, and Maria Korynsel wa North Palm Beach wakionyesha kumuunga mkono kwao Rais wa zamani Donald Trump March 30, 2023 baada ya kufunguliwa mashtaka.
Trang Le wa Orlando, kulia, and Maria Korynsel wa North Palm Beach wakionyesha kumuunga mkono kwao Rais wa zamani Donald Trump March 30, 2023 baada ya kufunguliwa mashtaka.

“Hatimaye. Alitakiwa awe amefunguliwa mashtaka kwa mambo milioni moja na yeye hatimaye amefunguliwa mashtaka kuhusu kitu fulani. Ni wakati hilo kufanyika! Alisema Caroline mkazi wa New York

Mkazi mwengine wa New York kwa jina la Oscar alisema anaamini mashtaka haya yatamsaidia Trump katika kuomba tena kuchaguliwa. “Hiki pengine ndicho wanachokitaka – kampeni ya Trump inataka hili. Ni soko huru. Atakuwa nje. Iwapo atashinda – fahamu, Nimeshinda! Nipigie kura!

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na Shirika la Habari la Associated Press.

XS
SM
MD
LG