Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 12:21

Trump adai atakamatwa Jumanne


Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump kupitia ujumbe wa mtandao wa kijamii Jumamosi amewaambia wafuasi wake kwamba kufuatia kile alicho kiita kuvuja kwa taarifa kutoka kwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa wilaya ya Manhattan, anatarajiwa kukamatwa Jumanne.

Katika ujumbe wake kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, ametoa mwito kwa wafuasi wake kuandamana kulirejesha taifa.

Hakuna uthibitisho kutoka kwa mamlaka zinazo husika wa uwepo wa mashitaka ya uhalifu yanayo mhusu Trump.

Ripoti za vyombo vya habari katika siku kadhaa zilizopita zimeeleza kwamba idara za kusimamia sheria za jiji la New York, zimekuwa jikijadili kuhusu mipango ya kiusalama endapo Trump atajisalimisha baada ya kukutwa na mashtaka ya kujibu.

Kama Trump atafunguliwa mashtaka rasmi, itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwa rais wa zamani kukamatwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG