Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 17:48

Nyaraka za siri zagunduliwa nyumbani kwa Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence


Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence
Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence

Nyaraka  zenye alama za siri zimegunduliwa  nyumbani kwa aliyekuwa  Makamu wa Rais Mike Pence huko Indiana  wiki iliyopita, wakili wake  ameiambia Idara ya  Hifadhi ya Taifa katika barua – ikiwa ni ugunduzi wa karibuni katika mfululizo wa nyaraka za siri ambazo zimekutwa kwenye makazi binafsi.

Rekodi “zinaonekana kuwa ni idadi ndogo ya nyaraka zilizowekewa alama za siri ambazo bila ya kukusudiwa ziliwekwa kwenye maboksi na kusafirishwa kwenda katika makazi binafsi ya makamu wa rais wa zamani mwishoni mwa utawala uliyopita,” wakili wa Pence, Greg Jacob, aliandika katika barua yake ambayo shirika la habari la The Associated Press iliipata.

Amesema kuwa pence “ alishirikiana na wakili wa nje, mwenye uzoefu wa kushughulikia nyaraka za siri , kuangalia rekodi zilivyokuwa zimehifadhiwa nyumbani kwake , baada ya kujulikana kuwa nyaraka hizo zenye alama za siri ziligundulika kwenye makazi ya Rais wa Marekani Joe Biden hukoWilmington.

Wizara ya Sheria tayari inatumia mwanasheria maalum kufanya uchunguzi wa kuwepo kwa nyaraka hizo zenye alama za siri zilizochukuliwa kutoka kwenye makazi ya Rais wa zamani Donald Trump huko Florida, na kutoka nyumbani kwa Biden na ofisi yake ya zamani ya Washington.

Wizara hiyo imesema takriban nyaraka 300 zenye alama, zikiwemo za kiwango cha juu cha siri zilichukuliwa kutoka Mar-a-Lago, na maafisa walijaribu kubaini iwapo Trump au mtu mwengine yeyote anapaswa kushitakiwa kwa kumiliki rekodi hizo kinyume cha sheria au kujaribu kuzuia upelelezi wa miezi kadhaa unaoendelea.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

XS
SM
MD
LG