Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:05

Wataalam wanaona kuna 'bomu' kwenye Wizara ya Sheria


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump 
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump 

Watalaam wanaona kuna ‘bomu’ kwenye Wizara ya Sheria Jumanne usiku katika kupokea maombi ambayo walisema waliidhinisha upekuzi wa FBI kwenye makazi ya rais wa zamani Donald Trump huko Florida.

Wamesema na pia kwenye klabu yake kwa sababu nyaraka nyeti za serikali ya Marekani huenda ‘zimefichwa na kuondolewa’ ili kuingilia kati uchunguzi.

Picha iliyotolewa kama kiambatanisho jana usiku katika maombi kwa wizara ya Sheria inaonyesha nyaraka zimesambazwa chini kwenye ofisi ya nyumbani ya Rais wa zamani Donald Trump kweye makazi yako huko Mar a Lago, na kuonyesha dhahiri unyeti wa nyaraka, kama mtaalamu mmoja alivyoiambia VOA.

Kimberly Wehle, Profesa wa Sheria, Chuo Kikuu cha Amerika anasema: “Nyaraka hizi kutoka kwenye picha zinajionyesha dhahiri kabisa, kulingana na jinsi alama. Zinavyoonyesha nje ya hizi nyaraka – ukiachangua na rangi ya machungwa – hizi ni nyaraka za siri.

Amedai au kupendekeza kwamba baadhi aliziondolea usiri wake. Hizi hazijawekewa alama kuwa zimeondolewa usiri wake. Na kwa kweli, bila ya ufafanuzi kama huo, bila ya kuzitenganisha, suala zima la uainishaji, haitakuwa vyema, kwasababu watu wanahitaji kufahamu kama ni za siri au si za siri.”

Upekuzi wa FBi wa Agosti 8 ambao haukutangazwa uliofanyika huko Mar-a- Lago umekuja baada ya mawakili wa Trump kusema mwezi Juni kwamba nyaraka zote za siri zimerejeshwa.

Makazi ya Rais wa zamani Donald Trump, Mar-a-Lago club, katika ufukwe wa Palm Beach, Fla., Aug. 31, 2022.
Makazi ya Rais wa zamani Donald Trump, Mar-a-Lago club, katika ufukwe wa Palm Beach, Fla., Aug. 31, 2022.

Wizara ya Sheria ilisema wakili wa Trump alitoa maelezo hayo “aliwazui wafanyakazi wa serikali kufungua au kuangalia kilichomo ndani ya maboksi yoyote ambayo yalibaki katika chumba cha hifadhi huko mar a Lago, na hakutoa fursa kwa serikali kuthibitisha kwamba hakuna nyaraka ambazo zilikuwa zimeandikiwa ni za siri zilizobaki huko.”

Mtaalamu mwingine alielezea kwanini hili linaweza kuwa tatizo kubwa kwa Trump na mawakili wake.

Bradley P. Moss, Mwanasheria wa Masuala ya Usalama wa Taifa:“Kilicho kibaya zaidi, sababu ambazo nadhani hii itasababisha kufunguliwa mashtaka, je kulikuwa na upinzani, kulikuwa na kuficha, kulikuwa na uingiliaji kati.

Kuzitafuta nyaraka zote huko Mar a Lago kuapa kwa FBI mwezi Juni kuwa kulikuwa hakuna rekodi zaidi. Na bado FBI, iliweza kuzitambua na kupata ushahidi kwamba kulikuwa na habari zaidi, kulikuwa na rekodi zaidi, na kwamba timu ya Trump ilikuwa ikificha hilo.”

Moss aliiambia VOA anaamini kuwa Trump huenda akakabiliwa na mshtaka ya uhalifu kutokana na nyaraka hizo, lakini haamini kuwa huenda mashtaka hayo yako karibu.

Moss ameongeza kuwa: “Huleti aina hii ya mashtaka mpaka uwe na uhakika wa kesi ambayo haitakuwa na mianya na una kila kuanzia I mpaka T umekishughulikia kwa kina. Sidhani wamefika katika hatua hiyo, lakini naamini watafika katika muda wa miezi michache ijayo.”

Wizara ya Sheria huenda ikafikiria athari za kisiasa kumshtaki rais wa zamani, lakini pia kuna wasi wasi wa usalama wa taifa, amesema Wehle.

Wehle ameeleza pia: Lakini katika mawazo yangu, jambo kubwa sana ambalo liko kwenye sahani ya FBI hivi sasa na pengine CIA na sehemu nyingine za vymbo vya usalama hapa Marekani, ni “Mungu wangu, tumeathirika kiasi gani?

Uvunjaji huu una uzito gani? Je Donald Trump alihamisha nyaraka kutoka Mar a Lago? Je kuna nyaraka nyingine za ziada ambazo hatuzifahamu ambazo bado anazo? Na swali kubwa ni je aliwawezesha madui wetu wa nje?”

Trump alikanusha kufanya kosa lolote lakini hajaelezea kwanini aliziondoa nyaraka za siri kutoka White House. katika posti zake kwenye mitandao ya kijamii, aliishambulia Wizara ya Sheria na FBI, akisema bila ya ushahidi wowote kwamba upekuzi ulifoanywa nyumbani kwake ulikuwa na ushawishi wa kisiasa.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Naye Rais wa Marekani Joe Biden alieleza kuwa: “Sasa inasikitisha kuona hapa mashambulizi mapya kwa FBI.”

Biden alishutumu mashambulizi ya baadhi ya warepublican kwa FBI, akisema wao ni watekelezaji wa sheria ambao maisha yao yanatishiwa kwa kufanya tu kazi zao. Biden pia alisema ataliacha suala la uchunguzi wa nyaraka alizonazo Trump kwa Wizara ya Sheria.

XS
SM
MD
LG