Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:26

Trump achunguzwa kwa uwezekano wa kukiuka Sheria ya Ujasusi


Taarifa iliyowasilishwa na Wizara ya Sheria katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani ya Wilaya ya  Kusini ya  Florida ikimfahamisha Jaji kwamba mawakili wa Rais wa zamani Donald Trump hawana pingamizi kwa hati ya upekuzi katika jengo la Trump Mar-a-lago kuwekwa wazi kwa umma.
Taarifa iliyowasilishwa na Wizara ya Sheria katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani ya Wilaya ya  Kusini ya  Florida ikimfahamisha Jaji kwamba mawakili wa Rais wa zamani Donald Trump hawana pingamizi kwa hati ya upekuzi katika jengo la Trump Mar-a-lago kuwekwa wazi kwa umma.

Wizara ya  Sheria ya Marekani inamchunguza Rais wa zamani Donald Trump kwa uwezekano wa kukiuka Sheria ya Ujasusi na uhalifu mwingine baada ya Idara ya  Upelelezi  (FBI) kukamata seti 11 za nyaraka za siri kutoka nyumbani kwake Florida, Mar-a-Lago, mapema wiki hii.

Mahakama ya Wilaya ya Marekani ya Wilaya ya Kusini ya Florida Ijumaa iliidhinisha kuwa wazi kwa hati ya kufanya upekuzi, ambao inataja makosa ya jinai matatu ya jinai ya serikali kuu ambayo Wizara ya Sheria inayafuatilia kama sehemu ya uchunguzi wake kwa Trump: ukiukaji wa Sheria ya Ujasusi, kuingilia kati sheria kuchukua mkondo wake na uhalifu wa kushikilia rekodi za serikali.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Hakuna yeyote aliyefunguliwa mashtaka ya uhalifu kwa wakati huu.

Risiti ya vitu hivyo kutokana na upekuzi uliofanywa inaonyesha kuwa wafanyakazi wa FBI walichukua zaidi ya maboksi 20 ya nyaraka ikiwemo zile zilizowekwa alama ya siri ya juu, siri na siri za kawaida, na pia vitu vilivyokuwa vimewekwa alama “Rekodi Muhimu za Urais,” “Nyaraka za Siri Hafifu,” picha na nyaraka zilizoandikwa kwa mkono.

Kulingana na hati ya upekuzi, maeneo ya kupekuliwa ni pamoja na ofisi ya Trump, “vyumba vyote vya kuhifadhi vitu, na vyumba vingine vyote au maeneo ndani ya nyumba zinazotumika au zilizoko kwa ajili ya matumizi” ya Trump na wafanyakazi wake na “ambapo maboksi au nyaraka zinaweza kuhifadhiwa, ikiwemo nyumba au majengo katika eneo hilo.”

Mwanasheria Mkuu Merrick Garland
Mwanasheria Mkuu Merrick Garland

Upekuzi huo uliidhinishwa na Mwanasheria Mkuu Merrick Garland, ambaye Alhamisi alisema kuwa Wizara ya Sheria “haichukulii uamuzi huu kwa uwepesi” na inapowezekana “itajizuia zaidi kuingilia faragha kama ni njia mbadala ya kupekua na kuufanya finyu upekuzi wowote unaofanyika.

Sheria ya Ujasusi

Sheria ya Ujasusi ya 1917 inakataza kupata taarifa, kurekodi picha au kunakili maelezo ya taarifa yoyote inayohusiana na ulinzi wa taifa kwa nia au sababu ukiamini kuwa taarifa hiyo inaweza kutumika kuidhuru Marekani au kwa ajili ya maslahi ya nchi yoyote ya kigeni.

Sheria hiyo inakwenda mbali zaidi ya shughuli za “ujasusi” ikihusisha makosa ya kutumia vibaya nyaraka za siri.

Haijalishi iwapo Trump hatimaye atafikia mgogoro wa jinai, kesi hiyo tayari inahatarisha usalama wa taifa, alisema mtafiti wa Chuo Kikuu cha Georgetown Paul R. Pillar, ambaye amefanya kazi na shirika la Ujasusi la CIA kwa miaka 28.

XS
SM
MD
LG