Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 18:12

Jopo la wabunge Marekani latoa matokeo ya uchunguzi wa machafuko ya 2021


Kamati Teule ya Bunge la Marekani Kuchunguza Shambulio la Januari 6 dhidi ya bunge la Marekani ikifungua kikao chake cha hadhara mjini Washington.
Kamati Teule ya Bunge la Marekani Kuchunguza Shambulio la Januari 6 dhidi ya bunge la Marekani ikifungua kikao chake cha hadhara mjini Washington.

Wamarekani watoa maoni yanayotafautiana kufuatia kikao cha kwanza cha hadhara cha Kamati ya bunge la Marekani iliyokuwa ikichunguza shambulio la Januari 6, 2021, kwenye jengo la Bunge la Marekani.

Kwenye kikao hicho cha utangulizi wa vikao kadhaa wajumbe wa kamati wanasema baada ya uchunguzi wao wamegundua kile walichokitaja kama jaribio la mapinduzi lililoongozwa na Rais wa zamani Donald Trump.

Baadhi ya raia wamarekani wanasema wameshangazwa na matokeo hayo ya awali huku wafuasi sugu wa Rais wa zamani Donald Trump wakiendelea kudai kuwa hiyo ni njama ya kumharibia sifa.

Kikao hicho cha saa mbili kwa njia ya televisheni, cha kwanza katika mfululizo uliopangwa mwezi huu, kilifuatia uchunguzi wa kina juu ya shambulio lililofanywa na wafuasi wa Trump baada ya rais huyo wa kushindwa katika uchaguzi wa rais wa 2020 kwa Rais Joe Biden na kuendesha kampeni ya kuzuia wizi.

Mbunge wa chama cha demokrat Bennie Thompson mwenyekiti wa kamati hiyo, amesema kwamba shambulio hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa lilikuwa "kilele cha jaribio la mapinduzi," akiongeza kusema kwamba ghasia hizo zilitokana na njama iliyoenea, yenye awamu nyingi iliyolenga kupindua uchaguzi na Trump alikuwa katikati mwa njama hiyo.

XS
SM
MD
LG