Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:56

Murdoch asema baadhi ya wachambuzI wa Fox "walithibitisha madai ya uongo ya uchaguzi


Britain Rupert Murdoch
Britain Rupert Murdoch

Mwenyekiti wa Shirika la Habari la Fox Rupert Murdoch amekiri kuwa baadhi ya wachambuzi wa Fox News walithibitisha madai ya uongo ya Rais wa zamani Donald Trump na washirika wake kuwa  uchaguzi wa urais wa 2020 ulikuwa umeibiwa.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Kadhalika amekiri kuwa yeye (mwenyekiti) hakuingilia kati kuzuia kuenezwa kwa madai hayo, kulingana na maelezo ya ushahidi uliowekwa wazi Jumatatu.

Madai hayo na jinsi kampuni ilivyoshughulikia hayo katikati ya kesi ya kashfa dhidi ya kituo kikubwa cha habari iliyowasilishwa na Dominion Voting Systems.

Nyaraka zilizofunguliwa hivi karibuni ikiwemo maelezo kutoka katika ushahidi ambao Murdoch alihojiwa juu yake iwapo alikuwa anafahamu kuwa baadhi ya watangazaji wa mtandao huo – Lou Dobbs, Maria Bartiromo, Jeanine Pirro na Sean Hannity – katika baadhi ya nyakati walithibitisha madai ya uongo ya uchaguzi. Murdoch alijibu, “Ndiyo. Walithibitisha hivyo.”

Ushahidi wa Murdoch ni wa hivi karibuni kuwasilishwa katika kesi ya kashfa ikionyesha wasiwasi katika mtandao uliokuwa na hadhi ya juu namna ulivyoshughulikia madai ya Trump wakati viwango vyake vikiporomoka baada ya kituo hicho kutangaza Joe Biden ameshinda Arizona, ikimkasirisha Trump na wafuasi wake.

XS
SM
MD
LG