Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:44

Umoja wa Mataifa ulichangisha dola bilioni 1.2 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Yemen

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alipohudhuria mkutano wa Barza la Haki za Binadam mjini Geneva. REUTERS
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alipohudhuria mkutano wa Barza la Haki za Binadam mjini Geneva. REUTERS

Umoja wa Mataifa ulichangisha dola bilioni 1.2 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa Yemen, lakini kiasi hicho kiko chini sana ya lengo la dola bilioni 4.3 lililowekwa na Umoja wa Mataifa kuisaidia nchi hiyo iliyokumbwa na vita.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliuambia mkutano wa wafadhili wa kimataifa mjini Geneva Jumatatu kwamba Marekani itatoa dola milioni 444 za misaada ya kibinadamu kwa Yemen mwaka huu, na kuwataka wafadhili wengine kuongeza michango yao.

Kiwango cha changamoto tunachokabiliana nacho kinatisha. Lakini natoa wito kwa kila mtu kuweka mtazamo wetu kwa watu tunaotaka kuwasaidia, alisema.

Blinken alisema kuwa uhaba wa fedha wa mwaka jana kwa Yemen ulilazimisha mashirika ya Umoja wa Mataifa kupunguza operesheni nchini humo, ikiwa ni pamoja na mgao wa chakula.

XS
SM
MD
LG