Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 20:05

Wizara ya sheria Marekani yasema Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushtakiwa


Trump alipokuwa katika hafla ya mwaka mpya nyumbani kwake Mar-a-Lago Palm Beach, Florida. REUTERS

Wizara ya sheria ya Marekani imesema Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushtakiwa na maafisa wa Polisi wa bungeni  waliojeruhiwa na wabunge Wademokrat juu ya uasi wa Januari 6, 2021 katika bunge la Marekani.

Msimamo wa wizara hiyo kwamba Trump hana kinga kutokana na kesi kama hizo ilibainika katika kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama ya rufaa ya serikali kuu iliyotolewa Alhamisi.

Maelezo hayo yaliwasilishwa na mawakili katika Kitengo cha kesi zisizo za jinai cha wizara ya sheria na haihusiani na uchunguzi tofauti wa kijinai unaofanywa na mwendesha mashitaka maalum wa wizara hiyo ili kujua ikiwa Trump anaweza kushtakiwa kwa mashitaka ya jinai kwa juhudi za kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 katika ghasia za bungeni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG