Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 07:57

Hakuna ishara ya wanajeshi wa Ukraine kujisalimisha kwa wingi


FILE - FILE PHOTO: Mandhari ya majengo yaliyoharibiwa na nyuma yake ni kiwanda cha chuma cha Azovstal upande wa kusini ya mji wa bandari wa Mariupol, Apr. 19, 2022.
FILE - FILE PHOTO: Mandhari ya majengo yaliyoharibiwa na nyuma yake ni kiwanda cha chuma cha Azovstal upande wa kusini ya mji wa bandari wa Mariupol, Apr. 19, 2022.

Wakati huo huo Moscow imeendelea na mashambulizi yake upande wa mashariki na serikali za Magharibi zimeahidi kutoa misaada zaidi ya kijeshi.

Maelfu ya vikosi vya wanajeshi wa Russia wakiwa na mizinga na roketi vilijaribu kusonga mbele katika kile ambacho maafisa wa Ukraine wanasema mapigano ya Donbas, ikiwa ni hatua ya mwisho Moscow kukamata majimbo mawili ya mashariki inayodai kwa niaba ya wanaotaka kujitenga.

Uvamizi wa Russia wa wiki nane umeshindwa kukamata miji yoyote mikubwa ya Ukraine.

Moscow ililazimika kuondoka kaskazini mwa Ukraine baada ya shambulizi la Kyiv kuzimwa mwezi uliopita, lakini imemwaga wanajeshi upande wa mashariki katika shambulizi lililoanza wiki hii.

Hili ni shambulizi kubwa kutokea kwenye taifa la Ulaya tangu mwaka 1945 ambalo limesababisha mamilioni ya watu kukimbia nje ya nchi na imeharibiwa na kuwa kama vifusi.

Russia imejaribu kuchukua udhibiti kamili wa Mariupol tangu siku za mwanzoni.

XS
SM
MD
LG