Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 06:48

Griffiths anakwenda Uturuki kwa juhudi za usitishaji mapigano Ukraine


Martin Griffiths mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu
Martin Griffiths mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu, Martin Griffiths, atasafiri kwenda Uturuki siku ya Jumanne kuendelea na juhudi zake za kufikia kiwango fulani cha usitishaji mapigano ya kibinadamu nchini Ukraine.

Sitisho la mapigano halionekanani kutokea hivi sasa, lakini yanaweza kuwa katika wiki kadhaa zijazo. Inaweza kuchukua muda mrefu kidogo zaidi ya hapo, Griffiths aliwaambia waandishi wa habari. Alisema inategemea vita vinaelekea wapi na namna mazungumzo kati ya Russia na Ukraine yanavyokwenda.

Mazungumzo hayo kwa sasa yanafanyika katika viwango vya chini sana. Griffiths pia alionyesha matumaini kwamba pasaka ya dhehebu la Orthodox hapo April 24 itaweza kutoa fursa ya kupumzika.

Wakati huo huo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alizungumza na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan siku ya Jumapili kuhusiana na juhudi za upatanishi zinazofanywa na Uturuki.

Guterres pia alisisitiza haja ya kuwa na njia za kibinadamu kwa ajili ya usambazaji wa misaada na kuwaondoa raia. Griffiths atafuatilia mjadala huo na Erdogan.

XS
SM
MD
LG