Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:06

Zelensky ayaomba mataifa ya magharibi kuiwekea Russia marufuku ya kuuza mafuta yake.


Wabunge wa Marekani wakitoa pongezi za dhati kwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Machi 16, 2022. Picha ya AP.
Wabunge wa Marekani wakitoa pongezi za dhati kwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Machi 16, 2022. Picha ya AP.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumatatu ameyataka mataifa ya magharibi kuiwekea haraka vikwazo vikali Russia, ikiwemo marufuku ya kuuza mafuta, ili kuizuia Moscow kuongeza bila pingamizi harakati zake dhidi ya Ukraine.

Katika hotuba yake ya kila usiku kwa wanainchi wa Ukraine kwa njia ya video, Zelensky aliyeonekana kuwa mwenye hasira amesema nchi za magharibi zilikosea mwaka jana kwa kuchelewesha vikwazo na uvamizi ulifuata.

“Vita kamili vimeanza. Sasa kuna vidokezo vingi na onyo zinazodaiwa kuwa vikwazo zaidi, kama vile marufuku ya uuzaji wa mafuta ya Russia barani Ulaya, itawekwa ikiwa Russia itatumia silaha za kemikali,” Zelensky amesema, akiweka mara kwa mara mikono yake juu ya meza.

Uvamizi wa Russia huko Ukraine ambao umedumu zaidi ya mwezi mmoja, mzozo mkubwa wa Ulaya tangu vita vya pili vya dunia, umepelekea zaidi ya Waukraine milioni 3.8 kukimbilia nchi jirani, huku ukiua maelfu ya watu na kujeruhi maelfu wengine, na kuitenga Russia kiuchumi.

Zelensky amesema vikwazo vinapaswa kuwa “vyenye ufanisi” na “vikali” kutokana na hatua za Russia kufikia sasa.

XS
SM
MD
LG