Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Russia yawataka wapiganaji wa Ukraine waliopo Mariupol kusalimisha silaha zao


FILE PHOTO: Mandhari ya kiwanda cha chuma cha Illich huko Mariupol, Ukraine kilivyo haribiwa na vita vya uvamizi wa Russia.
FILE PHOTO: Mandhari ya kiwanda cha chuma cha Illich huko Mariupol, Ukraine kilivyo haribiwa na vita vya uvamizi wa Russia.

Russia inasubiri Jumapili kwa wapiganaji wa Ukraine waliozingirwa katika mji wa bandari wa Mariupol kusalimisha silaha zao.

“Hakuna dalili yoyote ya wapiganaji wa Ukraine waliokwama katika kiwanda cha chuma cha Azovstal kinachoangaliana na Bahari ya Azov kutekeleza hilo,” kulingana na Reuters, saa kadhaa baada ya muda wa mwisho wa kujisalimisha wa saa 0300 UTC kumalizika.

Rais Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake Jumamosi usiku, “Hali katika mji wa Mariupol imebakia kuwa ni ya dharura. Na siyo ubinadamu… Russia kwa makusudi kujaribu kumuangamiza kila mtu aliyeko katika mji wa Mariupol.”

Iwapo Russia itaweza kuuteka mji wa Mariupol, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Russia kuuteka mji mkubwa wa Ukraine tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine Februari 24.

Zelenskyy alisema amezungumza na mawaziri wakuu wa Uingereza na Sweden Jumamosi kuhusu hali ilivyo Mariupol, vilevile kuhusu kuongeza vikwazo dhidi ya Russia, na ulinzi na msaada kwa ajili ya Ukraine.

Russia imeanza tena kushambulia kwa makombora katika maeneo kadhaa ya Ukraine, na pia kupiga mabomu katika miji mingine.

“Japokuwa tumesikia azma nyingi kutoka kwa wale wanaotaka kuisaidia” Ukraine kupambana na majeshi ya Russia, Zelenskyy alisema katika hotuba yake, hakuna katika hayo yaliyoweza kutekelezwa.

Bomu lililolipuka huko Kharkiv Jumamosi limeangamiza jiko la jamii lililokuwa limewekwa na Jiko la Kimataifa la Mpishi maarufu Jose Andres, ambalo linawalisha watu katika maeneo mbalimbali katika nchi ya Ukraine iliyoko katika vita na nchi jirani.

Andres ameliambia Shirika la habari la AP kuwa kikundi cha mpishi huyo kitaendelea kupika nchini Ukraine na shambulizi katika jiko hilo linaonyesha kuwa “kutoa chakula katikati ya vita visivyokuwa na busara ni kitendo cha ushujaa, ukakamavu na kujihami.”

Sehemu ya habari hii imetokana na vyanzo vya habari vya AP na Reuters

XS
SM
MD
LG