Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:15

UNHCR inasema takribani raia milioni tano wameondoka Ukraine


Baadhi ya wakimbizi wa Ukraine wakiondoka nchini mwao kwenda nchi jirani zilizo salama ikiwemo Poland
Baadhi ya wakimbizi wa Ukraine wakiondoka nchini mwao kwenda nchi jirani zilizo salama ikiwemo Poland

Katika kipindi cha chini ya miezi miwili tangu wanajeshi wa Russia walipoanza vita nchini Ukraine raia milioni tano wa Ukraine wameondoka nchini mwao na takribani milioni saba wamekoseshwa makazi ndani ya nchi kulingana na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR).

Wakimbizi wengi wa Ukraine wametafuta hifadhi katika nchi jirani za ulaya ambako wanapewa ulinzi wa muda na huduma mbalimbali. Wa-Ukraine sasa ni kundi kubwa la pili la wakimbizi duniani, wa pili baada ya wakimbizi zaidi ya milioni 6.8 wa Syria na wameongeza jumla ya idadi ya wakimbizi duniani hadi karibu milioni 32.

Vita hivyo pia vimewafanya watu milioni 7.1 wa Ukraine kuwa wakimbizi ndani ya nchi hiyo, idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani inayohusishwa na migogoro duniani. Vita vya Ukraine vimechochea mojawapo ya matukio ya kuhama kwa watu na matatizo ya kibinadamu yanayokua kwa kasi kuwahi kutokea Babar Baloch msemaji wa UNHCR aliiambia VOA.

XS
SM
MD
LG