Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:23

Gharama za maisha kuziathiri nchi za Afrika zaidi kuliko nchi tajiri


Greta Thunberg wa Sweden, kushoto, na watetezi wa hali ya hewa maarufu kama mtandao wa "Fridays for Future" movement wakifanya maandamano yasiyoruhusiwa siku ya kufunga Mkutano wa kila mwaka wa Jukwaa la Uchumi wa Kimataifa, WEF, Davos, Uswisi, Jan. 20, 2023.
Greta Thunberg wa Sweden, kushoto, na watetezi wa hali ya hewa maarufu kama mtandao wa "Fridays for Future" movement wakifanya maandamano yasiyoruhusiwa siku ya kufunga Mkutano wa kila mwaka wa Jukwaa la Uchumi wa Kimataifa, WEF, Davos, Uswisi, Jan. 20, 2023.

Katika nchi nyingi za Kiafrika, habari za mfumuko wa bei zinaonekana zilishika kasi mwaka jana na tayari zinapungua kasi, lakini hali ya kipekee kwa nchi zinazoendelea na zenye kipato cha chini barani Afrika, zinaweza kuendelea kuathiri maisha ya watu kwa mwaka mzima, wachambuzi waliokusanyika kwenye Jukwaa la kiuchumi la kimataifa (WEF) huko Davos, Uswisi wamesema wiki hii.

Kwa mfano, ukiangalia matumizi kwa chakula yalikuwa juu mno ya mapato ya kaya katika nchi zinazoendelea ukilinganisha na nchi tajiri, huku mishahara ikiwa chini, mathalan mgogoro wa gharama za maisha utakuwa mkubwa zaidi katika nchi za Afrika kuliko nchi tajiri.

Gita Gopinath, Naibu wa kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Fedha amesema bei zitabakia kuwa juu kwa takriban kipindi chote cha mwaka 2023 ingawa mfumuko wa bei unapungua, bei hazitashuka, ikimaanisha kuwa bei za bidhaa zinaendelea kupanda, taratibu na athari zinatofautiana kati ya nchi na kaya mbalimbali.

“Bei za vyakula zimeshuka, lakini bado ni asilimia 30 juu ya viwango vya mwaka 2019, tunaweza kuona kuwa bei za reja reja za vyakula zikipanda, hususan kwa katika nchi zinazoendelea” Gonipath amesema wakati akizungumza katika kikao cha Jukwaa hilo juu ya “Kuzuia Mgogoro wa Gharama za Maisha”(“Stemming the Cost-of-Living Crisis”) Jumanne.

Laura Tyson, profesa wa uchumi katika chuo kikuu cha California, Berkeley, amesema mfumuko wa bei wa vifungu vikuu vya gharama za maisha - chakula, makazi na nishati—vimeongeza tatizo la umaskini kote duniani wakati mishahara haikuongezeka inavyostahili.

“Tumeona ongezeko na siyo punguzo la idadi ya watu wanaoishi katika umaskini kwa sababu, mfumuko wa bei unaongeza tatizo ambalo lilikuwepo hapo awali na hatujalitatua,” amesema wakati wa kikao hicho cha Davos.

Hii taswira mbaya inaonekana katika eneo, ambapo licha ya mfumuko wa bei kuongezeka kwa kasi katika nchi nyingi Novemba mwaka jana, wananchi bado wanataabika na bei kubwa za vyakula na mafuta.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG