Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:17

Davos: Thunberg anajiandaa kukutana na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Nishati


Thunberg akamatwa na polisi Jumanne baada ya kushikiliwa pamoja na wanaharakati wengine wa hali ya hewa wakati wa maandamano nchini Luetzerath, Germany, Jan. 17, 2023.
Thunberg akamatwa na polisi Jumanne baada ya kushikiliwa pamoja na wanaharakati wengine wa hali ya hewa wakati wa maandamano nchini Luetzerath, Germany, Jan. 17, 2023.

Mwanaharakati wa mazingira Greta Thunberg anajiandaa kukutana na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Nishati Fatih Birol huko Davos Alhamisi, waandaaji wa mkutano wa tukio la kila mwaka la Jukwaa la Uchumi wa Dunia wameiambia Reuters.

Thunberg atakutana na Birol pamoja na wanakampeni wenzake Helena Gualinga, Vanessa Nakate na Luisa Neubauer, waandaajia walisema katika taarifa yao.

Shirika la IEA, ambalo huandaa mapendekezo ya sera juu ya nishati ulimwenguni, hawakuwa na maoni ya mara moja.

Thunberg aliachiwa na polisi Jumanne baada ya kushikiliwa pamoja na wanaharakati wengine wa hali ya hewa wakati wa maandamano nchini Ujerumani.

“Jana nilikuwa sehemu ya kundi mmoja lililokuwa likiandamana kwa amani dhidi ya upanuzi wa mgodi wa makaa ya m awe huko Ujerumani. Polisi walituzuia na kutuweka chini ya ulinzi lakini tuliachiliwa baadae jioni,” alituma katika ujumbe wa tweet, akiongeza: “kutetea hali ya hewa siyo uhalifu.”

'Hatupati ushindi'

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Al Gore alisema huko Davos kuwa anakubaliana na juhudi za Thunberg nchini Ujerumani na kwamba mgogoro wa hali ya hewa ulikuwa unazidi kuwa mbaya sana kuliko ulimwengu unavyojaribu kutafuta ufumbuzi.

“Hatushindi. Mgogoro huu bado unazidi kuwa mbaya sana kwa haraka kuliko tunavyoandaa njia za kutatua hayo,” Gore aliliambia jopo la WEF, akigusia kuongezeka mwanya kati ya wale “wenye umri mkubwa kuwa katika nafasi za uongozi na vijana wa dunia ya hivi leo.”

XS
SM
MD
LG