Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 01:46

Ramaphosa asitisha kuhudhuria kongomano la kiuchumi Uswizi kutoka na mzozo wa nishati nchini mwake


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefutilia mbali mipango ya kuhudhuria kongamano la kiuchumi duniani mjini Davos Uswizi kwa sababu ya mzozo wa nishati unaoiathiri nchi yake, msemaji wake amesema Jumapili.

Afrika Kusini inakumbwa na hali isiyo ya kawaida ya kukatika kwa umeme katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kutokana na matatizo kwenye kampuni ya serikali ya umeme ya Eskom.

Ramaphosa alikuwa anatarajiwa kuongoza ujumbe wa serikali kwenye mkutano huo mkubwa wa kiuchumi katika milima ya Uswizi wiki hii lakini badala yake atabaki nyumbani kufanya mazungumzo na Eskom na viongozi wa kisiasa, msemaji wake Vincent Magwenya amesema.

“Kutokana na mzozo wa nishati unaoendelea, Rais Cyril Ramaphosa amesitisha ziara yake kwenye kongamano la kiuchumi la dunia huko Davos,” Magwenya aliandika kwenye Twitter.

Amesema pia “Kwa sasa Rais ameitisha kikao na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni, kamati ya kitaifa ya mzozo wa nishati (NECCOM) na bodi ya Eskom.”

Ukataji wa umeme uliopangwa umekuwa ni mzigo kwa miaka mingi nchini Afrika Kusini, huku Eskom ikishindwa kuendana na kasi ya mahitaji na kukarabati miundombinu yake ya zamani ya nishati ya mkaa wa mawe.

Lakini, kukatika kwa umeme kulifikia kilele katika miezi 12 iliyopita, huku kampuni ya Eskom ikidai kwamba ni kutokana na hujuma na uhalifu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG