Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:00

Gambia: Wanajeshi wawili wa Senegal wauawa, tisa watoweka


Gambia Map
Gambia Map

Jeshi la Senegal limesema wanajeshi wake tisa wanaohudumu katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani nchini Gambia hawajulikani walipo.

Taarifa za jeshi zinasema kuna uwezekano wamechukuliwa mateka na waasi kutoka eneo la Casamance kusini mwa Senegal kufuatia mapigano.

Tangazo hilo la Jumanne limekuja siku moja baada ya jeshi kusema kuwa wanajeshi wawili wameuawa katika mapambano hayo hayo na wapiganaji wanaoaminika kuwa wanatoka kundi la MFDC.

Muasi mmoja pia ameuawa na wengine watatu wamekamatwa na wanajeshi wa Senegal katika mapigano ya Jumatatu, taarifa ya jeshi imesema.

Taarifa zinasema operesheni zinaendelea kuwasaka na kulinda eneo hilo.

Wanajeshi hao walikuwa wakifuatilia biashara ya mbao kama sehemu ya ECOMIG, tume ya kulinda amani kutoka jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi.

Kundi la MDFDC liliundwa mwaka 1982 kupigania uhuru wa Casamance.

XS
SM
MD
LG