Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:58

Chad haitofanya mazishi rasmi kwa Hissen Habre


Maafisa wa usalama wakishika doria kwenye barabara za mji mku wa Chad wa N'Djamena katika picha ya awali.
Maafisa wa usalama wakishika doria kwenye barabara za mji mku wa Chad wa N'Djamena katika picha ya awali.

Serikali ya Chad Jumanne imesema haina mipango yoyote ya kuandaa sherehe rasmi za kumuenzi rais wa zamani Hissen Habre ambaye alifariki kutokana na ugonjwa wa Covid 19, akiwa nchini Senegal ambako alikuwa anatumikia kifungo cha maisha kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

"Kufuatia uhalifu wake na kutowaheshimu waathiriwa wa vitendo vyake vya uhalifu, hakutokuwa sherehe rasmi za kumuenzi",, serikali ya Chad imeliambia shirika la habari la AFP.

Kiongozi huyo wa zamani wa Chad alifariki katika hospitali kuu mjini Dakar Jumanne, akiwa na umri wa miaka 79. Habre alichukua madaraka mwaka wa 1982, akiiongoza Chad kimabavu hadi alipokimbilia nchini Senegal mwaka wa 1990 baada ya kuondolewa madarakani na Idriss Deby Itno.

Uongozi wake uligubikwa na ukandamizaji wa kikatili dhidi ya wapinzani, ikiwemo madai ya mateso na mauaji holela ya wapinzani huku watu elfu 40 wanakadiriwa kuuawa,vitendo vilivyopelekea Habre kupewa jina la utani la “Pinochet wa Afrika”.

Msemaji wa serikali Abderaman Koulamallah amesema “ hatuna pingamizi yoyote kwa kuurejesha mwili wake nchini Chad, hata ingawa tunaungana pamoja na waathiriwa wote wa utawala wake”, akiongeza kuwa ni wajibu wa familia yake kufanya maamuzi.

XS
SM
MD
LG