Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 21:52

Rais wa zamani wa Chad afariki gerezani


Rais wa zamani wa Chad hayati Hissenne Habre
Rais wa zamani wa Chad hayati Hissenne Habre

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre, ambaye alikuwa katika kifungo  cha maisha nchini Senegal kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, amefariki dunia

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre, ambaye alikuwa katika kifungo cha maisha nchini Senegal kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, amefariki dunia Waziri wa Sheria wa Senegal Malick Sall alisema Jumanne. Habre alikuwa na miaka 79.

Habre yuko mikononi mwa mwenyenzi mungu, Bwana Sall alikiambia kituo cha televisheni cha TFM, wakati vyombo vya habari vilisema alikuwa amekufa kwa Covid-19.

Hissene Habre, ambaye aliitawala Chad kutoka 1982 hadi 1990, alihukumiwa Mei 30, 2016 kifungo cha maisha baada ya kesi iiliyofanyika mjini Dakar, na kukutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, ubakaji, mauaji, utumwa na utekaji nyara. Tume ya uchunguzi ya Chad ilikadiria idadi ya waathirika wa ukandamizaji chini ya utawala wa Habre ni 40,000.

Hissene Habre, aliyepinduliwa mwaka 1990, alikuwa alipata hifadhi nchini Senegal, ambapo, chini ya shinikizo la kimataifa, hati za kesi zake zilitayarishwa na ambapo alikamatwa mwaka 2013 na kushtakiwa na mahakama maalum iliyoundwa kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG