Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:39

COVID-19 : Tishio la watu kukataa kupewa chanjo laikabili dunia

Watu wakisubiri kupewa chanjo ya COVID-19, mjini Mumbai, India, Alhamisi, Aprili 29, 2021. India imeweka rekodi mpya ya maambukizi duniani ya kirusi kipya na nchi imeanza kuanzisha chanjo hiyo kwa watu wazima pamoja na changamoto nyingi.(AP Photo/Rajanish Kakade)

Matokeo ya ukusanyaji mpya wa maoni yanaonyesha kusita kwa baadhi ya watu kupewa chanjo kote ulimwenguni ni tishio katika kutokomeza janga la COVID-19.

Utafiti huo uliyoendeshwa na taasisi ya Gallup katika nchi 79 kati ya 117, unaonyesha kuwa idadi ya watu ambao wamesema wako tayari kupewa chanjo ni chini ya asilimia 70.

Idadi hiyo ndiyo asilimia ya wastani ya watu ambao wanahitaji kinga ili kuzuia virusi vya COVID visiendelee kusambaa, kwa mujibu wa wanasayansi.

Taasisi ya Gallup iliwahoji watu elfu moja katika kila nchi kati ya hizo 117 mwishoni mwa mwaka 2020.

Katika nchi 20, karibu watu wote waliohojiwa walisema hawako tayari kupewa chanjo.

Nchini Russia, asilimia 61, Kosovo asilimia 56 walisema wataikataa chanjo, na nchini Senegal ni asilimia 55.

Kulingana na matokeo ya jumla, utafiti huo unakadiria kuwa zaidi ya watu billioni 1 kati ya billlioni 7.6 duniani hawatachanjwa.

XS
SM
MD
LG