Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:07

Kenyatta alegeza masharti ya COVID-19 kaunti tano


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametangaza kuondoa katazo la watu kuingia au kutoka katika kaunti tano lililokuwa limewekwa kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Maeneo yaliyoathiriwa na katazo hilo yalikuwa ni Nairobi, Nakuru, Machakos, Kimabu na Kajiado.

Rais aliyasema hayo Jumamosi wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) mjini Nairobi.

Wakati alipotoa agizo la pili kwa umma mnamo Machi 2021, la jinsi ya kukabiliana na janga la Corona, Nairobi ilikuwa na jumla ya maambukizi 56,815.

Maambukizi yalipungua mwezi Aprili hadi 15,000, hii ikionyesha maambukizi yamepungua mjini Nairobi kwa asilimia 74, alisema.

Alisema takwimu za wataalamu wa afya zinaonyesha hali kama hiyo katika eneo ambalo "tuliweka amri ya watu kutotoka nje Machi 26, 2021."

"Baada ya mwezi mmoja wa marufuku ya kutoka nje, kesi za maambukizi ya COVID 19 zilipungua mpaka 72%," alisema Kenyatta.

Pia Rais amesema maeneo mengine ya nchi, maambukizi ya COVID yamepungua kwa 89% Mombasa na 90% Busia kati ya mwezi Machi na Aprili 2021.

XS
SM
MD
LG