Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:39

China : Marekani imefanya 'makosa' kuwafukuza wanadiplomasia


Geng Shuang
Geng Shuang

China mapema Jumatatu imeiomba Marekani kurekebisha "kosa" lake la kuwafukuza maafisa wake kutoka nchini.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Geng Shuang amesema shutuma dhidi ya maafisa wake waliokuwa Marekani zilienda kinyume na ukweli ulivyo na kuwa Marekani inahitaji kulinda ipasavyo haki za wanadiplomasia.

Geng aliyasema hayo mbele ya wanahabari baada ya kuulizwa swali kutokana na ripoti iliotolewa na gazeti la New York Times kwamba Marekani iliwafukuza kwa siri maafisa wawili wa China baada kuendesha gari hadi kwenye kituo kimoja cha kijeshi jimboni Virginia.

Ripoti hiyo imewataja watu wanaoelewa hali hiyo na imeeleza tukio hilo lilitokea mwishoni mwa septemba ambapo maafisa hao waliokuwa wameandamana na wake zao kwenye gari walifika katika lango la ukaguzi la kituo cha kijeshi na kuruhusiwa kuingia ndani ili waweze kugeuza gari lao na kutoka.

Hata hivyo inasemekana kuwa maafisa hao wa China waliendelea kuendesha gari bila kugeuza hadi walipokuta malori ya kuzima moto yaliokuwa yameziba barabara.

Gazeti la The Times limesema maafisa hao, mmoja kati yao alikuwa ni afisa usalama, walieleza kuwa walielewa vibaya maelekezo ya kugeuza gari wakiwa getini na hivyo kupotea.

Ripoti hiyo imesema maafisa wa Marekani wamekataa maelezo hayo na wanaliona tukio hilo ni jaribio la kupima usalama wa kituo hicho cha kijeshi.

XS
SM
MD
LG