Msemaji wa White House, Jen Psaki, aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kwamba Biden atataja njia sita zilizobuniwa kuwashawishi Wamarekani wengi kupata chanjo dhidi ya virusi pamoja na ushiriki wa sekta binafsi.
Hotuba ya Biden inakuja wakati Marekani inakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya COVID-19, kulazwa watu hospitalini na vifo vilivyosababishwa na maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Delta.
Utawala wa Rais Biden kwa miezi ya kwanza madarakani uliongeza juhudi zaidi kwa watu kupata chanjo ili kudhibiti kuenea kwa COVID-19.
Maambukizi mengi mapya yamekuwa kati ya Wamarekani ambao hawajapata chanjo, pamoja na idadi kubwa ya watoto wadogo, ambao hawastahili kupata chanjo.