Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 04:09

G20 kuimarisha juhudi za utoaji wa chanjo za Covid kwa mataifa masikini


Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen kwenye mkutano wa awali wa G20.

Kundi la nchi 20 tajiri duniani G20 Jumatatu limesema juhudi zaidi zinahitajika kuzisaidia nchi maskini kuchanja raia wao dhidi ya Covid 19, lakini hazikueleza wazi juu ya idadi mpya ya dozi au ahadi za dhati za msaada wa kifedha.

Italy ambayo ni mwenyekiti wa G20 mwaka huu imesema baada ya mkutano wa Roma ambao ulifanyika Jumapili na Jumatatu, kati ya mambo walioafikiana ni makubaliano ya kisiasa ili kuongeza msaada kwa nchi maskini na kuzipa chanjo zaidi.

“Kiwango cha ukosefu wa usawa katika ugavi wa chanjo ni cha juu sana na hali haiwezi kuendelea hivyo,” waziri wa afya wa Italia Roberto Speranza amewambia waandishi wa habari.

“Ikiwa tutaiacha sehemu ya dunia bila chanjo, kuna hatari ya kukabiliwa na aina mpya ya virusi ambavyo vitatuathiri sote.

Ujumbe wetu uko wazi, hakuna yeyote wa kuachwa nyuma katika kampeni ya kutoa chanjo,” ameongeza.

Chanjo zinasafirishwa kwenye nchi maskini kupitia mpango wa kimataifa wa COVAX, unaoungwa mkono na shirika la afya duniani (WHO) na mpango wa chanjo na kinga duniani (GAVI).

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG