Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:27

Wafanyakazi wa serikali ya zimbabwe wanaokataa chanjo ya Covid watakiwa kujiuzulu


Raia wa Zimbabwe wapanga foleni kupokea chanjo ya Covid-19.
Raia wa Zimbabwe wapanga foleni kupokea chanjo ya Covid-19.

Wafanyakazi wa serikali nchini Zimbabwe ambao hawataki chanjo dhidi ya COVID-19 wanapaswa kujiuzulu, waziri wake wa sheria Ziyambi Ziyambi amesemaalisema Jumanne.

Taifa hilo la kusini mwa Afrika hadi sasa limewachanja watu milioni 2.7, ingawa linalenga kuchanja theluthi mbili ya wakazi wake milioni 15, kufikia mwishoni mwa mwaka. Serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa inasema imelipia dozi milioni 12 za COVID-19 kutoka China.

Ziyambi amesema ingawa Wazimbabwe hawatalazimika kupata chanjo, wale walio katika utumishi wa umma walikuwa na jukumu la kulinda umma kwa kupata chanjo za COVID-19.

"Hatulazimishi chanjo lakini ikiwa wewe ni mfanyikazi wa serikali, kwa usalama wa wengine na watu unaowahudumia, pata chanjo," Ziyambi aliambia kituo kimoja cha redio, nchini humo.

Hakudokeza kwamba mamlaka itawaadhibu wafanyikazi wa serikali ambao wanakataa chanjo hiyo, lakini akasema wanapaswa kuchukua jukumu la wao kuacha.

"Ikiwa unataka kufurahia haki zako, ambazo ziko kwenye katiba, unaweza kujiuzulu," alisema.

Serikali ya Zimbabwe inaajiri zaidi ya watu 200,000, huku walimu wakiwa ndio wengi zaidi.

Ziyambi amesema "utafika wakati ambao hatutataka mwalimu yeyote ambaye hajachanjwa."

Shirikisho la vyama vya Wafanyikazi wa Sekta ya Umma la Zimbabwe, ambalo linawakilisha wafanyikazi wa serikali, limesema litatoa maoni baadaye.

Chanjo sasa zinapatikana kwa watu wazima wote nchini Zimbabwe, lakini vifaa ni vichache na zahanati hazina wafanyikazi wengi, haswa katika mji mkuu Harare, ambapo mara nyingi wakazi hulazimika kupanga foleni kutoka asubuhi na mapema kwa matumaini ya kupata chanjo.

XS
SM
MD
LG