Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:21

Biden alihutubia Bunge la Ireland, Spika asifia imani, busara, na uvumilivu wake


Rais wa Marekani Joe Biden akipiga picha za selfie na wageni baada ya kuhutubia Chuo Kikuu cha Ulster, Belfast, Ireland ya Kaskazini, April 12, 2023.

Wakati akiendelea na ziara yake rasmi ya siku nne huko Ireland Kaskazini na Jamhuri ya Ireland, Rais Joe Biden alizungumza katika bunge  mjini Dublin.

Biden ni rais wa nne wa Marekani baada ya John F. Kennedy, Ronald Reagan na Bill Cinton kuzungumza katika kikao cha pamoja cha bunge la Ireland.

FILE - Rais John F. Kennedy (AP Photo)
FILE - Rais John F. Kennedy (AP Photo)

Katika kile ambacho kimelezewa kurejea ‘nyumbani’ huko Dublin, alizungumza kwenye bunge la Ireland.

Rais wa Marekani, Joe Biden alikumbushia kuhusu urithi wake wa Iralenda na kuangazia uhusiano wa kudumu na Ireland ambao ulianza na kuanzishwa kwa Marekani.

Rais Joe Biden amesema kuwa: “Mioyo ya Wairish imesaidia kuangaza tochi ya ukombozi katika nchi yangu na moto wa azma ya mapinduzi, damu ya wa Ireland kutoka kote katika kisiwa hiki kwa hiari yao waliitoa kwa ajili ya uhuru wa nchi yangu.”

Vita vya Ukraine

Biden alipongeza uungaji mkono wa Dublin katika kuitetea Ukraine kutokana na uvamizi wa Russia.

Ireland, sehemu ya Umoja wa Ulaya lakini si mwanachama wa NATO, jeshi lake halielemei upande wowote lakini linatoa msaada wa kibinadamu kwa Ukraine.

Mapema Biden alimshukuru Waziri Mkuu wa Ireland Leo Varadkar kwa kuwakaribisha takriban wakimbizi elfu 80 wa Ukraine.

Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu Leo Varadkar katika ofisi ya Farmleigh House, April 13, 2023, Dublin.
Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu Leo Varadkar katika ofisi ya Farmleigh House, April 13, 2023, Dublin.

Leo Varadkar, Waziri Mkuu wa Ireland alieleza kuwa: “Na pia tunathibitisha azma yetu kwamba Ireland na Marekani na Ulaya ni vyema zisimame pamoja katika kupendelea demokrasia na ukombozi katika dunia, ambayo inashambuliwa kutoka kila upande.”

Amefanya hivyo katika kipindi chote cha ziara yake, ambayo ilianza Jumanne mjini Belfast, Ireland Kaskazini.

Biden katika hotuba yake alipongeza Mkataba wa Good Friday makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 1998.

Ambayo yalisaidia kumaliza miaka 30 ya mzozo wa umwagaji damu juu kama Ireland Kaskazini iungane na Ireland au ibaki kama sehemu ya Uingereza.

Alipokuwa akipiga kengele huko mapema jana Alhamisi, Biden kwa mara nyingine tena alielezea matumaini ya kurejeshwa kwa mpango wa kushirikiana madaraka huko Ireland Kaskazini, ambao ulivunika kutokana na malumbano ya ndani ya kisiasa, na kuhatarisha makubaliano ya amani.

Alisema Uingereza na Ireland ni vyema zifanye kazi pamoja kuepuka kurejea kwa umwagaji damu.

Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak huko Belfast. REUTERS/Kevin Lamarque
Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak huko Belfast. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais Joe Biden alieleza:“Ghasia za kisiasa zisiruhusiwe kwamwe kuwepo katika kisiwa hiki.” Hotuba ya Biden ilipokelewa kwa hisia kali kutoka kwa wabunge,

Seán Ó Fearghaíl, Spika wa Baraza Kuu la Bunge anaeleza: “Umeonyesha imani yako isiyotetereka, ustahmilivu mkubwa sana na uwezo wa kuwaleta pamoja watu mbali mbali na mara nyingi wenye maoni tofauti.”

Na kwa Mary Heanye, mke wa marehemu Seamus Heaney, ambaye alikuwa mshairi, na kazi yake mara kwa mara Biden aliiizungumzia.

Alimaliza siku yake kwa dhifa ya chakula cha jioni ambacho kiliandaliwa na mwenyeji wake Varadkar, katika kasri ya Dublin.

Ripoti hii imetayarishwa na mwandishi wa White House Patsy Widakuswara na imetokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

XS
SM
MD
LG