Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:58

Makamu wa Rais wa Marekani asema Marekani itaongeza uwekezaji barani Afrika

Majkamu rais wa Marekani Kamala Harris alipozungumza katika hafla ya kusherehekea Mwezi wa Historia ya Weusi katika White House, Februari 28, 2022, huko Washington.
Majkamu rais wa Marekani Kamala Harris alipozungumza katika hafla ya kusherehekea Mwezi wa Historia ya Weusi katika White House, Februari 28, 2022, huko Washington.

Maka.mu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alisema Jumapili kwamba Marekani itaongeza uwekezaji barani Afrika na kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wakati alipokuwa akianza ziara ya wiki moja barani humo inayolenga kukabiliana na ushawishi wa mpinzani wake China

China imewekeza fedha nyingi barani Afrika katika miongo ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na maendeleo ya miundo mbinu na rasilimali wakati ushawishi wa Russia pia umeongezeka ikiwa ni pamoja na kutumwa kwa wanajeshi kutoka kwa mkandarasi binafsi wa kijeshi wa Russia Wagner Group kuzisaidia serikali katika nchi kadhaa.

Katika safari hii naakusudia kufanya kazi ambayo imejikita katika kuongeza uwekezaji hapa barani na kufanikisha ukuaji wa uchumi na fursa. Harris alisema mara baada ya kuwasili nchini Ghana ikiwa ni sehemu ya kwanza katika safari ambayo itampeleka hadi nchini Tanzania na Zambia.

Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden umetaka kuimarisha uhusiano na Afrika kwa sehemu ili kutoa njia mbadala kwa mataifa yanayohasimiana.

XS
SM
MD
LG