Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 17:47

Marekani kuisaidia Ghana na nchi nyingine kupunguza madeni


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo wakati akihudhuria dhifa ya taifa wakati wa ziara yake nchini Ghana.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo wakati akihudhuria dhifa ya taifa wakati wa ziara yake nchini Ghana.

Marekani itaendelea kuwasukuma wakopeshaji ili kupunguza madeni ambayo kuna tija  kwa nchi ambazo zinahitaji, ikiwemo Ghana, alisema hayo Makamu Raia wa Marekani Kamala Harris wakati wa ziara yake katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Khadija Riyami. Khadija Riyami.

Kamala Harris alizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari akiwa pamoja na rais wa Ghana Nana Akufo Addo. Mapema mwezi wa Machi, Akufo Addo alisema kwamba wafanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha huenda likaipa Ghana mpango wa mkopo kwa bodi yake ya utendaji ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Harris pia alitangaza msaada wa dola milioni 100 kusaidia kuzuia mzozo na juhudi za kuleta uthabiti huko Benin, Ivory Coast, Ghana, Guinea na Togo.

Makamu wa Rais alisema: “Kusaidia kushughulikia vitisho vya ghasia zenye msimamo mkali na ukosefu wa uthabiti, leo, napenda kutangaza msaada wa dola milioni 100 kwa Benin, Ghana, Guinea, Ivory Coast na Togo. Wiki iliyopita, Rais Joe Biden alitangaza mpango wa mkakati kwa pwani ya Afrika Magharibi kama sehemu ya mkakati wa Marekani kuzuia mzozo na kuhamasisha uthabiti. Leo, ufadhili na tangazo hili ambalo nimelitoa itasaidia utekelezaji wa mpango huo, na kushughulikia utawala usalama na masuala ya maendeleo katika eneo hilo.”

Washington kupeleka mshauri

Washington pia itampeleka mshauri nchini Ghana kutoka ofisi yake ya kiufundi ili kuisaidia nchi hiyo kuboresha “uhimilivu wa deni na kusaidia katika ushindani, soko la deni la serikali,” ofisi ya Harris ilisema.

Ghana ilishindwa kulipa kiasi kikubwa cha deni lake la nje la takriban dola bilioni 29 mwaka jana, wakati malipo ya riba na mfumuko wa bei ulipanda, nab ado inahitaji kufanya mashauriano kupata suluhisho kwa wamiliki wa kimataifa binafsi wa bondi na wakopeshaji.

China ni mkopeshaji mkubwa sana wa Ghana huku ikiwa na deni la takriban dola bilioni 1.9. Wizara ya fedha ya Ghana ilisema wiki iliyopita kuwa ilitarajiwa kupata uhakikisho ‘haraka sana’ kufuatia mikutano yake nchini China.

Rais wa Ghana apongeza uungaji mkono mageuzi

Nana Akufo-Addo, Rais wa Ghana anaeleza: “Nimeridhishwa kusema kwamba makamu rais Harris ameahidi uungaji mkono wa Marekani katika ajenda hii ya mageuzi. Ni mageuzi haya ambayo yatatupa fursa ya kupata mafanikio makubwa kutokana na rasilimali zetu za asili nyingi sana, kutuwezesha kuwa na msingi thabiti wenye maana kwa kipindi kirefu cha uchumi na uhusiano wa kibiashara na Marekani.”

Harris alitembelea studio ya muziki mjini Accra ambako alijiunga na waigizaji Idris Elba na Shery Lee Ralph.

Wakati akiitembelea studio ya vibrate, Harris aliangazia lugha ya kimataifa inayohusika katika kuandaa muziki kutoka kwa wasanii vijana wa kiafrika.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani: “Kinachotokea hapa ni kubadilika jinsi watu wanavyofurahi wenyewe na nadhani wanavyojielezea. Kuna mengi sana kuhusu uwezo wetu wa kupokea muziki ni kuhusu kuipokea lugha ya kimataifa, na hicho ndiyo tunakifanya hapa, unazungumza kwa njia ambayo kote duniani watu wanasikia nyimbo ambazo zimejikita katika dhana kama vile uhuru.”

Muigizaji Idris Elba

Muigizaji Idris Elba anasema Kamala Harris ziara yake katika bara h ilo inakuza ushirikiano na uwekezaji.

Idris Elba, Muigizaji: “Nadhani ina umuhimu mkubwa, ni ishara, makamu rais kwenda Ghana, kwenda Afrika. Na kuwepo na muingiliano, unajua, kuionyesha dunia kwamba kwa hakika ni sehem nzuri kuiangalia katika misingi ya ushirikiano na uwekezaji.”

Makamu rais ni mjumbe muhimu katika utawala wa Rais Joe Biden kuitelembea Afrika mwaka huu, na atakwenda hadi Tanzania na Zambia wiki hii. Ziara yake ni sehemu ya juhudi pana za Marekani zinazofanywa wakati China na Russia wamekita maslahi yao kwenye bara hilo la AFrika.

XS
SM
MD
LG