Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:51

Benki za maendeleo za matafa tajiri kuwekeza $80 bilioni Afrika


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwenye mkutano wa kiongozi wa G7 huko Carbis Bay, Cornwall, Uingereza, Juni 12, 2021. Leon Neal/Pool via REUTERS
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwenye mkutano wa kiongozi wa G7 huko Carbis Bay, Cornwall, Uingereza, Juni 12, 2021. Leon Neal/Pool via REUTERS

Benki kubwa za maendeleo za mataifa tajiri duniani Jumatatu zimeahidi kuwekeza dola billioni 80 kwenye makampuni ya Afrika na miradi katika miaka mitano ijayo.

Shirika la kimataifa la fedha (IMF) lilikadiri kuwa nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara zitahitaji msaada wa ziada wa billioni 425 kati ya hivi sasa na 2025.

Msaada huo utatumika kupambana na janga la COVID-19 na kupunguza viwango vya umaskini vilivyoongezeka kutokana na janga hilo.

Kanda hiyo imetaabika sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na ni kwa mara ya kwanza taasisi za maendeleo kutoka Marekani, Ulaya na nchi nyingine tajiri za kundi la G7 kutoa ahadi ya pamoja ya dola billioni 80 kwa bara la Afrika.

David Marshik, afisa mkuu kwenye taasisi ya Marekani inayohusika na ufadhili wa maendeleo ya kimataifa, anasema kuwekeza zaidi barani Afrika hivi sasa ni kipaumbele chini ya utawala wa Rais Biden.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG