Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:28

Marekani kutangaza mkakati mpya wa ufadhili wa miundombinu


Rais wa Marekani Joe Biden ahudhuria mkutano wa G7 huko Carbis Bay, Cornwall, Juni 11, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden ahudhuria mkutano wa G7 huko Carbis Bay, Cornwall, Juni 11, 2021.

Utawala wa Rais wa Marekani, Joe Biden umesema utatangaza mkakati wa ufadhili wa miundombinu kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.

Mkakati huo ambao umetengenezwa kushindana na ule wa hasimu wake China unaojulikana kama Belt and Road Initiative.

Juhudi hiyo itaitwa, “Build Back Better for the World,” umezinduliwa leo Jumamosi pamoja na washirika wa G7 katika mkutano unaofanyika Cornwall, Uingereza.

Mkakati huo utakuwa na msukumo thaminio, uwazi na endelevu” kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa utawala wa Biden.

Belt and Road Initiative ni mkakati wa mendeleo wa ulimwengu ulioanzishwa na Beijing mwaka 2013, na kuwekeza katika nchi karibu 70. Ni kiini cha sera yake ya mambo ya nje.

Afisa mwandamizi wa Marekani amesema mkakati wa ‘B3W’ kama unavyoitwa unalenga kuhamasisha sekta binafsi ili kuwekeza na kutimiza ufadhili wa trilioni ya dola katika miundo mbinu ambayo inahitajika katika dunia inayoendelea, wakati ikikidhi mahitaji ya ajira na viwango vya mazingira na uwazi.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG