Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 14:58

Ajali ya magari matano yauwa watu 32 Uganda


Ramani ya Uganda

Magari matano katika barabara kuu magharibi mwa Uganda, usiku wa kuamkia Jumatano yamesababisha vifo vya watu 32, na kujeruhi wengine watano katika ajali tofauti. 

Irene Nakasiita, msemaji wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Uganda, amesema kwamba ajali hizo zimetokea katika barabara ya Fort Portal na Kasese ambayo kwa sasa ipo katika ujenzi.

Taarifa za awali zinaonyesha kwamba lori lililokuwa limebeba maiti kwenda mazikoni liligongana na gari jingine kabla ya gari la tatu lililokuwa limebeba watu kadhaa nalo kugonga magari hayo.

Kadhalika magari mengine mawili ambayo madereva wake walipoteza mwelekeo na kujikuta yanangonga na magari kadhaa yaliyo gongana awali.

Polisi bado wanashughulikia sababu ya ajali hizo nchini Uganda, ambayo huandikisha vifo vya watu 2,000 kwa mwaka kutokana na ajali hizo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG