Duru za habari zinaarifu kuwa abiria na wafanyakazi wote walitolewa kwa ndege hiyo iliyokuwa ikichomeka.
Picha za televisheni zilionyesha miali ya moto ikitokea kwenye madirisha na sehemu ya ndani ya ndege ya shirika la ndege la Japan Airlines wakati wazima moto wakipambana na moto huo.
Vyombo vya habari vya Japan viliripoti kuwa ndege hiyo ilitua katika uwanja wa Haneda ikitokea kwa uwanja wa ndege wa Shin-Chitose huko Hokkaido, zaidi ya kilomita 1,200 kaskazini mwa Tokyo, ikiwa na abiria 379 na wafanyakazi.
Taarifa zilieleza kwamba ndege hiyo huenda iligongana na ndege ya walinzi wa pwani ya Japan.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa wafanyakazi watano kati ya sita waliokuwa kwenye ndege ya walinzi wa pwani walithibitishwa kufariki.
Forum