Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:11

Meli karibu na Yemen imeelezwa kuripoti shambulizi la droni, milipuko Bahari ya Sham


Ramani ikionyesha eneo la Bahari ya Sham, Israel, na Yemen ambako kumekuwa na mashambulizi ya meli za mizigo katika eneo la Pwani ya Yemen.
Ramani ikionyesha eneo la Bahari ya Sham, Israel, na Yemen ambako kumekuwa na mashambulizi ya meli za mizigo katika eneo la Pwani ya Yemen.

Milipuko miwili imeripotiwa kwenye bahari ya Sham katika meli iliyokuwa ikisafiri nje ya pwani ya Yemen siku ya Jumanne muda mfupi  baada ya ndege zisizokuwa na rubani kuonekana, mamlaka ya usafiri wa baharini  ya Uingereza imesema.

Milipuko hiyo ilitokea kiasi cha kilomita 9 kutoka katika meli kwenye eneo la Bahari ya Sham kilomita 93 kutoka bandari ya Hodeidah iliyoko pwani ya magharibi mwa Yemen, taasisi ya Uingereza ya United Kingdom Maritime Trade Operations (UKMTO) ilisema katika taarifa yake.

Utambulisho wa meli hiyo, maelezo ya mzigo iliyobeba au ilikuwa inaelekea wapi au ilikotokea havikutajwa.

UKMTO ilisema kuwa chombo hicho kilikuwa na mawasiliano na majeshi ya ushirika na meli hiyo na mabaharia wake waliripotiwa wako salama.

Meli hiyo inaelezewa kuendelea na safari yake.

Tukio hilo lililoripotiwa limekuja wiki moja baada ya Marekani kutangaza juhudi za kimataifa za usalama wa baharini katika eneo la Bahari ya Sham kukabiliana na mashambulizi yanayofanywa na Wahouthi wa Yemen dhidi ya meli.

Wanamgambo wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wameshambulia meli za biashara zinazo fanya safari katika bahari hiyo tangu mwezi Oktoba, kampeni ambayo kikundi hicho kinasema ni kwa ajili ya kuwaunga mkono Wapalestina waliozingirwa na Israel huko Gaza.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG