Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 02:30

Mamlaka ya Japani yawataka watu kuhama maeneo ya pwani magharibi

Wanunuzi wakiinama huku tetemeko la ardhi likipiga eneo hilo katika duka kubwa la Toyama
Wanunuzi wakiinama huku tetemeko la ardhi likipiga eneo hilo katika duka kubwa la Toyama

Mamlaka ya Japani iliwataka watu kuhama maeneo ya pwani magharibi mwa Japan baada ya tetemeko kubwa la ardhi leo Jumatatu alasiri kusababisha tahadhari kubwa ya tsunami.

Mamlaka ya Japani iliwataka watu kuhama maeneo ya pwani magharibi mwa Japan baada ya tetemeko kubwa la ardhi leo Jumatatu alasiri kusababisha tahadhari kubwa ya tsunami.

Inakadiriwa kuwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Rikta lilitokea kwenye pwani ya Ishikawa na kufuatiwa na takriban matetemeko 20 katika saa zilizofuata, mengi yakiwa ya kiwango cha 5.

Shirika la Hali ya Hewa la Japan lilitoa maonyo ya tsunami kwa wilaya za Ishikawa, Niigata na Toyama.

Shirika hilo lilikadiria tsunami yenye mawimbi yenye urefu wa mita tano yanaweza kupiga Ishikawa. Ililipa eneo hilo onyo la kiwango cha juu zaidi, ambalo halijatolewa tangu tetemeko la ardhi la mwaka 2011 na tsunami iliylioharibu eneo la kaskazini mashariki mwa Japan.

Forum

XS
SM
MD
LG