Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:56

Mlipuko katika ghala ya mafuta Guinea wadhibitiwa


Moto ukiwaka katika ghala kubwa ya mafuta iliyopo katika mji wa Conakry nchini Guinea. Picha na STRINGER / AFP
Moto ukiwaka katika ghala kubwa ya mafuta iliyopo katika mji wa Conakry nchini Guinea. Picha na STRINGER / AFP

Mlipuko na moto uliotokea katika ghala kuu ya mafuta iliyoua watu 24 na kujeruhi 454 “umezimwa kabisa” siku tisa tangu moto huo uanze, ilisema taarifa ya serikali kwa shirika la habari la AFP.

Moto huo tayari umedhibitiwa, lakini siyo kikamilifu.

“Zoezi la kupooza mitambo yote ya petroli linaendelea” na eneo la ajali linaendelea kufungwa ili kuruhusu uchunguzi ufanyike”

Miongoni mwa watu 24 waliofariki, 11 hawajatambuliwa na waliojeruhiwa, 31 bado wanapatiwa matibabu hospitali na 423 wameruhusiwa.

Ubora wa hewa umeongezeka, serikali ilisema, lakini uvaaji wa barakoa bado unapendekezwa.

Usambazaji mafuta ulianza tena siku ya Jumamosi kwa kuweka kiwango cha lita 25 kwa gari na lita 5 kwa usafiri wa magari ya magud=rudmu mawili au matatu. Kujaza mafuta kwenye madebe kumepigwa marufuku.

Malori ya mafutai hayatasindikizwa na polisi.

Kulinga na hesabu za awali, takribani majengo 800 yaliharibiwa mengi miongoni mwa majengo hayo ni yaliyokuwa ndani ya mita 500 linalolizunguka eneo la ajali.

Serikali imetoa vifaa vya afya 450 kwa lengo la kusambaza kwenye kaya 2,141 zilizoathiriwa, taarifa hiyo imesema.

Jumla ya watu 11,000 wameathiriwa na moto huo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG