Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:35

Nigeria inatoa wito kuachiliwa kwa Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Bazoum


Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum katika picha iliyochukuliwa huko Niamey. May 2, 2022.
Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum katika picha iliyochukuliwa huko Niamey. May 2, 2022.

Nigeria ni mwenyekiti wa sasa wa jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ambayo imeiwekea vikwazo Niger kufuatia mapinduzi ya Julai yaliyomuondoa madarakani Bazoum.

Nigeria inatoa wito wa kuachiliwa huru kwa Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum na utawala wa kijeshi ili kumruhusu kuondoka kwenda nchi ya tatu, waziri wake wa mambo ya nje amesema.

Nigeria ni mwenyekiti wa sasa wa jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ambayo imeiwekea vikwazo Niger kufuatia mapinduzi ya Julai yaliyomuondoa madarakani Bazoum.

ECOWAS ilidai Bazoum arejee madarakani mara moja lakini utawala wa kijeshi ume-endelea kumuweka kizuizini na kusema huenda ukahitaji hadi miaka mitatu ili kurejesha utawala wa kiraia.

“Tunawaomba wamuachie Rais Bazoum ili aruhusiwe kuondoka Niger”, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Tuggar, ameiambia Channels TV, katika mahojiano yaliyochapishwa kwenye tovuti yake wikiendi.

“Hatokuwa tena chini ya ulinzi. Atakwenda katika nchi ya tatu ambayo inakubaliwa na pande zote. Na kisha tutaanza kuzungumzia kuondolewa kwa vikwazo”.

Nembo ya ECOWAS
Nembo ya ECOWAS

Alisema ECOWAS bado iko wazi kwa mazungumzo na serikali ya kijeshi ya Niger.

“Unajua, fursa hii ipo. Wakati wote tuko tayari, tuko tayari, na tunaweza kuwasikiliza na mpira uko mikononi mwao”.

Viongozi wa ECOWAS watakutana katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, Desemba 10 kujadili masuala ya eneo hilo, ambako tangu mapinduzi ya mwaka 2020 yameweka utawala wa kijeshi nchini Mali, Burkina Faso, Guinea na Niger.

Mwezi uliopita, jaribio la mapinduzi lililoshindwa lilisababisha vifo vya watu 21 nchini Sierra Leone, mwanachama mwingine wa ECOWAS kulingana na maafisa waandamizi nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG