Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 18:29

Iraq inalaani mashambulizi ya anga ya Marekani ikiyaita "kitendo cha chuki"


Mfano wa ndege isiyotumia rubani-Drone
Mfano wa ndege isiyotumia rubani-Drone

Serikali ya Iraq imeyaita mashambulizi ya Marekani kuwa ukiukaji usiokubalika wa uhuru wa Iraq

Iraq imelaani mashambulizi ya anga ya Marekani ya Jumanne katika eneo la Iraq, na kukiita “kitendo cha chuki” na ukiukaji wa uhuru wa Iraq.

Vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi hayo siku ya Jumatatu na kuwalenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq, katika kujibu shambulio la ndege zisizokuwa na rubani mapema siku hiyo ambazo ziliwajeruhi wanajeshi watatu wa Marekani.

Mashambulizi ya Marekani yamemuua mmoja wa wanajeshi wake, Iraq imesema Jumanne na kuwajeruhi watu wengine 18, wakiwemo raia. Serikali imeyaita mashambulizi ya Marekani kuwa ukiukaji usiokubalika wa uhuru wa Iraq, taarifa ya serikali imesema.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa mashambulizi kama hayo yanayofanywa na makundi yenye silaha dhidi ya washauri wa muungano unaoongozwa na Marekani, ni vitendo vya uhasama na yanakiuka uhuru wa Iraq, msimamo ambao Kataib Hezbollah aliukosoa.

“Tunawaonya wale wenye roho dhaifu, kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini, wasijaribu kuchokoza uvumilivu wetu”, alisema Abu Ali al-Askari, afisa wa usalama wa kundi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG