Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, wameitisha maandamano kulalamikia kile wamedai kama kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Kenya na utawala mbovu. Rais William Ruto ametishia kukabiliana na waandamanaji kwa nguvu zote. Ruto, ametoa wito kwa Odinga kufanya mazungumzo na serikali kwa kuheshimu sheria zilizopo na wala sio kutumia maandamano ambayo mara nyingi huambatana na vifo na uharibifu wa mali