Lakini siku ya Ijumaa - siku nne baada ya tetemeko hilo – manusura kadhaa walitolewa kutoka kwenye magofu katika jimbo la Hatay kusini mwa Uturuki, akiwemo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 na mama yake.
Maafisa wanasema idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililopiga mkoa wa mpakani kati ya Uturuki na Syria siku ya Jumatatu imefikia zaidi ya watu 21,000, na kufanya kuwa ni tetemeko baya zaidi la ardhi kuwahi kutokea tangu lile la tsunami la mwaka 2011 ambalo lililouwa takribani watu 20,000 nchini Japan.
Juhudi za vikosi vya uokoaji zinakwamishwa na ukosefu wa vifaa.
Mpaka Alhamisi, msafara wa malori sita ya msaada ya Umoja wa Mataifa kupitia kivuko cha Bab al-Hawa, kivuko pekee ambacho Umoja wa Mataifa umeidhinisha kutumika kupeleka misaada ya kibinadamu kutoka Uturuki kwenda kaskazini mwa Syria yameshindwa kufikia maeneo ambayo hayako chini ya utawala wa Syria.
Barabara inayoelekea kwenye kivuko upande wa Uturuki iliyoharibiwa na tetemeko hilo ilikuwa ndio kwanza limefunguliwa tena.
Maeneo ya utafutaji pia yamekuwa na sherehe kiasi watu wanapopatikana wakiwa hai na kupelekwa kupatiwa matibabu. Lakini kufukua vifusi pia kumemaanisha kuongezeka haraka kwa idadi ya vifo.