Baada ya usiku ambapo vipimo vya hali ya hewa vilipungua hadi kwenye hali ya baridi, kulikuwa na mitetemeko mingi zaidi siku moja baada ya tetemeko hilo la kipimo cha 7.8.
Zaidi ya mitetemeko 20 kati ya hiyo ilikuwa na kipimo cha 4.0 au zaidi, na kutikisa eneo lililo kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ameelezea uungaji wake mkono kwa wanainchi wa Uturuki na Syria katika “kipindi hiki cha huzuni mkubwa,” na amesema idadi ya vifo haizingatii “huzuni na hasara zinazopitia familia hivi sasa ambazo zimepoteza baba, mama, binti, mtoto chini ya vifusi, au ambazo hazijuwi kama wapendwa wao wako hai au wamekufa.”
Akizungumza kwenye mkutano wa WHO mjini Geneva, Tedros amesema shirika hilo linatuma ndege za kukodi na vifaa vya matibabu kwa nchi zote mbili na kwamba litafanya kazi kuwasaidia watakapopata afueni na kujenga upya.
Facebook Forum