Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 23:00

Ebola Uganda: Madaktari wanasusia kwenda kazini kutokana na ukosefu wa vifaa


Jane Apunyo, kiongozi wa wauguzi katika hospitali ya Mubende, akiwa kazini saa za usiku, kwenye kituo cha kutibu wagonjwa wa Ebola.
Oct 27 2022
Jane Apunyo, kiongozi wa wauguzi katika hospitali ya Mubende, akiwa kazini saa za usiku, kwenye kituo cha kutibu wagonjwa wa Ebola. Oct 27 2022

Madaktari nchini Uganda wanasusia kwenda kazini kutokana na hofu ya kuambukizwa virusi vya Ebola kwa sababu hawana vifaa maalum vya kuwajinga na maambukizi, kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika, na kuchelewa kupata mshahara.

Madaktari 15 wameambukizwa Ebola nchini Uganda na 6 wamefariki.

Uganda inakabiliana na mlipuko wa virusi vya Ebola aina ya Sudan ambayo haina chanjo.

Jumla ya watu 141 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola na 55 wamefariki.

Shirika la afya duniani WHO na makundi mengine ya kutoa msaada yanaendelea kutoa msaada kwa Uganda kukabiliana na Ebola. Marekani imetoa msaada wad ola milioni 22 kupitia kwa washirika wake nchini Uganda.

Wizara ya afya ya Uganda imesema kwamba kuna uhaba wa wafanyakazi wa afya na vifaa kupambana na Ebola.

XS
SM
MD
LG