Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:59

WFP yasema eneo la Sahel barani Afrika linakabiliwa na njaa


Watoto wakitembea kwenye mchanga wa jangwa eneo la Sahel, May 25 2012.
Watoto wakitembea kwenye mchanga wa jangwa eneo la Sahel, May 25 2012.

Shirika la mpango wa chakula Duniani la Umoja wa Mataifa linasema eneo la sahel barani Afrika linakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula ambao haujawahi kushuhudiwa unaosababishwa na kupanda kwa bei, harakati za kigaidi, mahitaji makubwa ya kikanda na COVID-19. Mwakilishi wa WFP nchini Birkina Faso anaonya kwamba hali ni mbaya huku mamilioni ya watu watakabiliwa na njaa katika miezi ijayo.

Katika maeneo makubwa ya Burkina Faso, vikundi vya kigaidi vyenye uhusiano na Islamic State na al-Qaida hutembea kwa uhuru mashambani, wakishambulia raia pamoja na vikosi vya usalama.

Mchanganyiko wa vigezo mbali mbali vibaya unasababisha bei ya chakula kupanda katika eneo lote, kulingana na program ya chakula duniani (WFP).

Wizi wa mifugo unaofanywa na makundi ya kigaidi, ni sababu mojawapo, anasema Antoine Renard, mkurugenzi wa WFP nchini Burkina Faso.

“Kuna mahitaji makubwa katika kanda, kwa hivyo hicho ni kipengele kimoja katika suala la mwelekeo wa soko. La pili, ni migogoro na bila shaka ina athari namna ya jinsi unavyoweza kuvuna. Una weza vipi kuendelea kuhakikisha kwamba masoko yako juu na yanaendelea na biashara huko Burkina Faso. Na mwisho, ni athari za kiuchumi za COVID-19”.

WFP inasema rekodi inaonyesha watu milioni 28 wana ukosefu wa usalama wa chakula huko Afrika magharibi na kati.

Pia inasema nchini Burkina Faso, Mali na Niger, njaa inaweza kuongezeka kwa asilimia 50 katika miezi ijayo, kutoka milioni 5.5 hadi zaidi ya milioni 8.

XS
SM
MD
LG