Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 13:05

Kwaheri 2020, Karibu 2021


Baada ya mwaka wa aina ya kipekee ambao kwa wengine ni mwaka wa ajabu, hatimaye watu katika sehemu mbali mbali za dunia wanajitayarisha kuuaga na kukaribisha mwaka mpya wa 2021, kwa matumaini kwamba utarejesha utulivu na mafanikio.

Tayari Australia imeingia mwaka 2021 kwa sherehe kubwa zilizohusisha kufyatua fataki, katika mji wa Sydney.

Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya nchini Australia, ambayo huwa nchi ya kwanza kukaribisha mwaka mpya, huwa zinafuatiliwa sana kote duniani.

Roketi za fataki zimefyatuliwa kutoka jumba maarufu la Opera, na kuunda upinde angani wa rangi mbalimbali zenye maandhari ya kuvutia kabisa.

Hata hivyo, kinyume na miaka iliyopita, hakukuwa na watu wengi kushuhudia sherehe hizo kutokana na hatua za kudhibithi maambukizi ya virusi vya Corona.

XS
SM
MD
LG